Sunday, June 13, 2021

MUNGU ANAPENDA AKUFUNULIE ANACHOKIFANYA

 MUNGU ANAPENDA AKUFUNULIE ANACHOKIFANYA



*Amosi 3:7*

_[7]Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lo lote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake._



Bwana Yesu asifiwe wapendwa. Leo napenda nikutie moyo kwamba Mungu anapenda akujulishe kile anachokifanya kwenye maisha yako na kile anachofanya kinachohusu maisha yako.


Ukisoma Amosi 3:7 anasema, Bwana hatafanya *neno lolote* bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.


Maana yake kila kitu ambacho Mungu anataka kufanya lazima kwanza awafunulie watumishi wake.


Kwenye Agano la Kale Mungu aliweza kuongea na manabii tu kwa sababu wao walijiliwa na Roho wa Bwana lakini kwenye Agano Jipya Mungu anaongea na kila mtu aliye na Roho Mtakatifu.


1 Wakorintho 2:10

_[10] *Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho.* Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu._


Kila kitu Mungu anachotaka kukufunulia anakufunulia kwa kupitia Roho Mtakatifu. Kwa hiyo kama una Roho Mtakatifu basi una uhalali wa kufunuliwa siri za Mungu na kujua mambo ambayo Mungu anataka ayatende kwenye maisha yako.


Ukisoma pia Yohana 16:13 Yesu alisema, Roho Mtakatifu atatupasha habari za mambo yajayo.


Maana yake ukiwa na Roho Mtakatifu una uwezo wa kujua Mungu atakufanyia nini kesho na utajua pia nini ufanye ili kile Mungu anachotaka kufanya kwako kitimie.


Ni muhimu ujifunze kujua ni vitu gani Mungu anataka afanye kwako ili pia uweze kujua vitu ambavyo havitoki kwa Mungu ili uvikatae.


Watu wengi wanakubali kila kitu kitokee kwenye maisha yao kwa kufikiri kuwa ni mapenzi ya Mungu lakini sio kweli.


Mungu ameahidi kukujulisha kwanza kabla hajafanya neno lolote. Lakini shetani yeye atafanya lolote bila kukujulisha ndio maana Neno linasema *tukeshe* ili tuweze kumpinga shetani. 


1 Petro 5:8-9

_[8] *Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.*_

_[9] *Nanyi mpingeni huyo, mkiwa thabiti katika imani,*_

 

Kwa hiyo ukiona kitu kibaya kinataka kutokea ambacho Mungu hajakujulisha usikubali hata kidogo. 


Kazi mojawapo ya maombi ni kuruhusu mapenzi ya Mungu na kukataa kila kitu ambacho sio mapenzi ya Mungu.


Mpendwa usiwe mlegevu kwenye maombi kwa sababu unaweza ukashindwa kupata kitu ambacho Mungu anataka upate ila pia ukiwa mlegevu kwenye maombi kuna mambo yatatokea kwako ambayo sio mapenzi ya Mungu kwako.


 ```Kwa hiyo; JIFUNZE KUOMBA KWA BIDII BILA KUKATA TAMAA``` .


_Mungu ameahidi kutofanya neno lolote bila kukujulisha. Kwa hiyo ukiona kitu kinatokea ambacho huna taarifa kutoka kwa Mungu ujue sio Mungu kwa hiyo kataa hicho kitu kwenye maombi._

 ```

Mpendwa natamani leo uongoze kumsikia Mungu anasema nini.


Mungu hatafanya neno lolote bila kukujulisha kwanza. 


Maana yake kutokujua kwako ni kizuizi cha Mungu kufanya kitu fulani kwenye maisha yako.


Kwa mfano Mungu akitaka AKUPONYE; Atakufunulia kwanza na kukujulisha kwamba yeye ni MPONYAJI halafu ukisha-amini na kujua kuwa Bwana anataka akuponye hapo ndipo anakuponya kwa sababu hatatenda neno lolote bila kukufunulia na kukujulisha.``` 


Thank You🙏🏽



*Pastor Baraka Malachi*

No comments:

Post a Comment