Wednesday, August 28, 2013

USINGIZI WA KIROHO * sehemu ya tatu*

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee…

KULALA KIROHO
*Ni ile hali ya kujisahau kufanya mazoezi ya UTAUWA
( hali ya kujisahau kukaa katika uwepo wa Bwana.)

*Mtu yeyote Yule asiyekaa ndani ya UWEPO wa Mungu basi ni dhahili kabisa atakuwa katika UWEPO wa shetani

Kwa jambo hilo hakuna hali ya uvugu uvugu,yaani ikiwa mtu hatakuwepo katika ufalme wa Mungu basi jibu ni kwamba atakuwepo katika ufalme wa shetani,hakuna ufalme wa VUGU VUGU.

Binadamu aliumbwa kwamba akae katika uwepo wa Mungu muda wote,maana hapo ndipo pana maisha ya kweli kama vile samaki akaavyo katika uwepo wa maji.
Endapo utamtoa samaki katika maji basi ujue atakufa tu,alikadhalika kwa mtu ambaye ametolewa katika uwepo wa Mungu ,ujue naye ni lazima afe,afe kifo cha kiroho.

Mtu alipo lala kiroho,aliruhusu Adui aamke na kuja kupanda uwepo wake kwa sababu zipo falme mbili hapa Duniani
*Ufalme wa Nuru
*Ufalme wa giza

Labda tuendelee kujifunza juu ya ile habari ya wale makahaba wawili,tuone ilikuwaje;(Kumbuka tulikuwa tumeishia mstari wa 21,katika 1 Wafalme sura ya 3)Sasa tunaendelea na mstari wa 22.

Tunasoma 1 Wafalme 3 :22
“ Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.”

*Adui hujaribu kwa KUTUMIA NGUVU ZAKE kubadilisha ukweli kwa uovu juu ya kile ulichopewa na Bwana Mungu.
Tazama andiko hilo vizuri jinsi yule mama ambaye mtoto wake aliyekufa akijaribu kumshindikiza mwenzake akubaliane naye kiwepesi wepesi.

Jiulize ni mara ngapi unabadilishiwa vitu vyako halisi kwa vitu feki,pindi ulalapo kiroho?
Labda unaweza usijue haya mambo kiurahisi maana shetani naye ni mjinga kwa sababu yeye huja kama malaika wa Nuru ili pindi ajapo kukubadilishia mambo yako usimgundue na uone ni sawa tu.

*Lakini leo Sio wakati wa kukubali kiurahisi rahisi tu.

Oooh,!
Jina la Bwana libarikiwe sana…

Nampenda yule mama mwenye haki,Kwa maana alisema HAPANA! si kweli katika maelezo ya ADUI alipeleka naye maelezo yake mbele ya mfalme.
Leo tunaye mfalme wetu,Pindi uonapo mambo si shwari baada ya mbadilishano uliotokea usiku,
nawe usisite kwenda mbele ya mfalme ambaye ndie YESU KRISTO WA NAZARETI

Nakuambia mpelekee mashtaka yako,peleka na kile kilichobadilishwa tena mpeleke na huyo adui/shetani mwambie twende msalabani tukashtaki,
kisha uone.

Katika mstari wa 23
Tunasoma ;
1 Wafalme 3 :25
“ Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu.”

*Hapa tunajifunza kwamba,Mfalme wetu Bwana Yesu ,mfalme wa Amani yeye hana upendeleo ,Yeye huamua kwa HAKI kwa maana yeye ni mwenye haki na mtakatifu sana.

Adui alifurahia sana kusikia mtoto yule aliye hai kwamba atakatwa kwa upanga hadi kufa.
Kwa maana alijua kwamba watakosa wote.Lengo lake ni kunyang’anya mtoto ambaye si wake.

*
Na hivi ndivyo hali ilivyo kwa shetani katika maisha yetu kila siku .Yeye shetani/Adui hufurahia pale unapopoteza kile kizuri.
Lakini ninakuambia Mungu wetu ambaye ni mfalme Yeye atahukumu kwa haki tu,
Tazama ikiwa Adui ameshika tumbo lako katika ulimwengu wa roho kwa kukubadilishia KIZAZI kwamba USIZAE,Leo hii ninakutangazia UTAZAA katika jina la Yesu Kristo,ni jambo la kuamini tu,na inawezekana.

Kumbuka ;
Watu hao ni makahaba tu ,
watu waliohasi mbele za Bwana
Lakini Biblia inasema walimuendea mfalme kwa ajili ya kupata haki.

*Hata wewe uliye mdhambi leo ninakuambia bado ipo nafasi ya kumuendea Bwana Mfalme kwa kuomba TOBA kisha kumpelekea mashtaka yako uliyobadilishiwa wakati ulipokuwa katika ufalme wa giza,kwa maana ulipokuwa umelala kiroho ndio kipindi ulipokuwa katika ufalme wa giza.

*Ikiwa makahaba walimuendea Bwana naye Bwana akaamua kwa haki, JE SI ZAIDI SANA KWAKO WEWE AMBAYE SI KAHABA?

*ninakuomba usikose kabisa fundisho hili katika sehemu ya nne,
maana natamani hata kama ning’eliweza kuongea na wewe moja kwa moja,Nitakapomaliza fundisho hili nitafanya maombi kwako ukiwa utahitaji mawasiliano 0655 111149

ITAENDELEA…

UBARIKIWE.

No comments:

Post a Comment