Bishop YONA P SOLA LEMA Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL 0754049163 |
(Kiongozi ni wa muhimu sana, Kiongozi lazima ajue
njia (Roho anajua Zab: 32: 8a)
- Mungu anatumia
njia mbalimbali kuongoza watu wake
-Jinsi ya
kuongozwa na roho.
A.
Watu wengi
wanajikuta katika hali ambazo hatujui tufanye nini lakini Mungu anayo majibu
kwa ajili yetu.
-Mungu
amepanga wale walio katika Yesu waongezwe na Roho wake.
-kama tunataka tuone mafanikio katika maisha yetu, lazima
maisha yetu yaongozwe na Roho na
yawezeshwe na Roho.
B.
Mmojawapo ya
mambo yenye kuvunja moyo mno hapa duniani ni watu kuwa katika wokovu lakini
wasijue jinsi ya kuongozwa na Roho.
Mungu
ametupa Roho wake ili atusaidie tufanye maamuzi sahihi.
1.
Tunapokabiliwa na
mateso.
2.
Kuudhiwa.
3.
Mashambulizi ya
Kiroho
4.
Shinikizo la
mawazo.
-Tunapotaka
kununua ardhi, kujenga ,kuwasaidia watu, kuhubiri ,kuoa ,kuolewa, kusema,
kunyamaza yaongozwe na Roho.
-Tunahitaji msaada
wa Roho wa Mungu sana.
- Roho yupo
kutusaidia tufanye vizuri (Rum 8:26)
-Roho hukaa kwa
mtu mtii na mnyenyekevu (Mat 5:32)
-Tumepewa Roho
wake ili tufanye maamuzi yanayofaa.
-Ni vizuri
tujifunze jinsi ya kumsikiliza Roho wa Mungu.
-Ili uwe mwana wa
Mungu kubali kuongozwa na Roho wake (Rum 8:14)
-
Kama huna Roho wewe
siyo wa Yesu (Rum 8: 9)
-
Maamuzi uliyowahi
kuchukuaga uliongozwa na Roho, kazi uliyonayo au uliyowahi kuifanya ukaacha
uliongozwa na Roho?
-
Maamuzi
tunayofanya bila kuongozwa na Roho yatatugharimu sana.
-Kadri ulimwengu
unavyoendelea na mambo yake, sisi tunapaswa tumsikilize Mungu sana.
-
Andiko toka:-
Torati 4: 5-6 Neno ni hekima hekima zetu na akili zetu.
MUNGU ANATUONGOZA KUPITIA NENO LAKE LILILOANDIKWA:
- Neno la Mungu
lililoandikwa ni Hekima ya Mungu (Luka 11: 49)
- Je unahitaji
hekima ya Mungu kwa ajili ya maisha yako au nyumba yako, kazi yako, Biblia
ndiyo mahali pa kwanza pa kutafuta.
A.
Watu wanapokosa
mwelekeo wataupata kwenye neno la Mungu.
Neno
la Mungu liliandikwa linatuhakikishia Kufanikiwa katika maisha yetu kile
tunachotaka kukifanya (Yosh 1: 7-8)
Mungu
alimpatia mwelekezo ili huduma yake iwe na mafanikio.
Mwana
alimwambia ulitafakari neno lake
usiku na mchana.
Tafuta
majibu yote ya maisha yako katika neno la Mungu.
Ayubu
alilitunza neno la Mungu kuliko riziki yake (Ayubu 23:12).
Neno
linamulika njia yetu (Zab 119: 105 , 128 Mf, Mama Jusi na nyota.
Mungu
anatuongoza kwa neno lake.
B.
Ukitaka maisha
yako yapendeze na kufanikiwa weak maisha yako juu ya neno (Mawazo, maamuzi,
utendaji) Zab 119: 9-10.
Roho
awaongoza katika kweli yote ya neno la Mungu (Yoh 16: 13, 17: 17).
C.
Tafuta kwanza
neno la Mungu linasemaje kabla yaw ewe kufanya maamuzi.
Mf,
Ibrahim na Lutu/ alifanya maamuzi kuondoka na ndugu yake akamwuliza Mungu, Lutu
alikuwa shida na watumishi wake katika safari, ugomvi kila siku.
Huyo
rafiki uliyenaye ulimpata kwa Mungu, mfanya kazi, mume, mke kwa uongozi wa
Mungu.
Wakati
tunapoenda kando na neno ndipo tunatumbukia.
MUNGU ANATUONGOZA KWA AMANI YAKE
NDANI YETU (KOLOSAI 3: 15)
-
Tujifunze
kuruhusu amani ya Mungu ikuongoze (acha ijenge ngome ndani yako).
-
Amani iamue na
mkate shauri kikamilifu yanayoinuka katika nia ya akili zenu.
-Unapoanza kuomba
kuhusu kufanya jambo, jiulize kama una amani
moyoni mwako au unasitasita huna hali ya kutulia.
-Unataka kufanya
biashara, kusomea ujuzi Fulani, unataka kuoa/kuolewa na Fulani n.k.
-Ukienda katika
njia ya hekima kutakupelekea kwenye amani (Mith 3: 13 – 17).
-Jua majaribu ya
Mungu ni amani (Njia zote Mungu aweza kupitisha matumaini hata kama zina mateso).
-Maamuzi mengi
makubwa yanaweza kufanywa kwa misingi ya Amani.
-Roho wa Mungu
aweza kukataza au kukuzulia jambo Fulani uwe makini mf, (Mat 16: 6).
ITAENDELEA...
ITAENDELEA...
MUNGU akubariki sana
by Bishop YONA P SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
No comments:
Post a Comment