Wednesday, August 28, 2013

SABABU TANO(5) ZA MTU KUSHINDWA KATIKA MAJARIBU


Nikiwa na Mchungaji Elly Boto baada ya ibada ya ubatizo  huko kawe beach.


Kila mwanadamu kuna wakati hupitia katika majaribu ya aina mbalimbali katika maisha yake. Kuna majaribu ambayo huja kwa sababu ya kupungua kwa maombi, kuna majaribu yanayotokana na hila za watu, kuna majaribu yanayotokana tamaa ya mtu mwenyewe  na pia kuna majaribu kama kipimo cha MUNGU kwa mtu wake ampendae.
*Swali ni kwanini tunashindwa katika majaribu?
zifuatazo ni sababu 5 za mtu kushindwa katika majaribu na hapa tunajifunza kwa kupitia  mtumishi wa MUNGU Ayubu.

SABABU 5 ZA MTU KUSHINDWA KATIKA JARIBU.
1:Wahudumu wetu katika majaribu.
Ayubu 2:9.''Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu, ukafe''
 Hapa mke wa Ayubu ambaye alitakiwa awe ndiye anayemtia moyo mmewe yeye ndio kwanza alimwambia amkufuru MUNGU ili afe. Na hata leo wapo watu wengi sana ambao yawezekana uko kwenye jaribu fulani mfano ugonjwa lakini wao ndio kwanza ushauri wao kwako ni kwamba uende kwa mganga wa kienyeji ukawekewe jini ili upate nafuu kumbe ndio kabisa wanakupoteza. Hivyo  wahudumu kwenye jaribu wanaweza kabisa wakasababisha ushindwe katika jaribu fulani hata kama ni dogo.

2:Marafiki tunaoshilikiana nao au wanaotutembelea wakati wa tatizo.
Ayubu 2:12-13''

Basi walipovua macho yao, nao wakali mbali, wasimtambue, wakainua sauti zao na kulia; kila mmoja akararua joho yake, wakarusha mavumbi juu ya vichwa vyao kuelekea mbinguni. Kisha wakaketi nchi pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lo lote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.''
 Marafiki wakati mwingine wanaweza kuwa kikwazo cha mtu kushinda jaribu alilonalo na hapa tunajifunza kuhusu marafiki watatu wa ayubu ambao walikuja kumtembelea  na badala ya wao kuwa faraja ndio kwanza walianza kumshutumu Ayubu kwamba haiwezekani awe hivyo lazima tu kuna dhambi amefanya na wanamwambia awaambie dhambi aliyofanya ili wamwombee kwa MUNGU na jaribu lake liishe kumbe wao ndio wakosaji na sio Ayubu.ndugu ni mara ngapi umepatwa na magumu na marafiki zako kuanza kukushutumu kwamba haiwezekani MUNGU ayaruhusu hayo kwako ni lazima tu umetenda dhambi kumbe hata dhambi hukutenda ila ni jaribu tu la kupima imani yako na baada ya kushinda jaribu hili unapandishwa kutoka utukufu hadi utukufu. Hivyo marafiki au watu wanaokutembelea wakati wa jaribu wanaweza kuwa sababu yako ya kushindwa kama ukiamua kuwasikiliza wakuambiacho. Hapa ayubu hakuwapa nafasi ndio maana alishinda majaribu hayo.
Unaweza ukajiuliza kati ya Ayubu na wale rafiki zake ni nani alikua  na mashaka? Marafiki zake walikua na mashaka kuliko hata mgonjwa mwenyewe na kama uko kwenye hali mbaya harafu wazima waliokuzunguka wao ndio wanalia hata wanashindwa kula hakika watazidisha ugonjwa kwako muhusika kamili.

3:Kujihesabia haki wakati wa majaribu.
Ayubu 9:2
''Kweli najua kuwa ndivyo hivyo; Lakini mtu huwaje mwenye haki mbele za Mungu?''
 usijihesabie haki wakati wa jaribu na pia ndugu waliochini kiroho  usiwasikilize sana wakati wa jaribu maana imani zao ni ndogo hivyo ni rahisi sana kukukatisha tamaa na kukupelekea uchukue maamuzi mabaya tena ukiwa karibu kabisa na ushindi wako.

4:Tusijilinganishe sana na wale ambao hawajaribiwi wakati huo. Ayubu 12:4
''Mimi ni mtu wa kuchekwa na jirani yake, Ni mtu niliyemwita Mungu, naye akanijibu; Huyo mwenye haki, aliye mtimilifu, amekuwa ni kicheko''
 Ndugu usikubali  kujiringanishi na watu ambao hawajaribiwi wakati huo maana unaweza ukaanza kulalamika na kupelelea kukufuru kwa MUNGU na kuona kama unaonewa wewe tu huku wengine wakiishi kwa amani na furaha isipokua wewe tu.

5:Tusiwahusudu wasioamini.
ukiwahusudu wasioamini utakuwa unajipoteza wewe mwenyewe pia ukiwahusudu wasioamni utakua unaanza kuikataa mbingu.

HAYA YOTE HUPUNGUZA UWEZEKANO WA KUSHINDA MAJARIBU.
MUNGU awabariki sana .
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

No comments:

Post a Comment