JEREMIA 1: 4
– 10
Ø Ulishawahi kujiuliza ulizaliwa
kwa kusudi gani?
Ø Ujana ni zawadi kutoka kwa Mungu.
Ø Mungu anajua umuhimu wa Kijana na
shetani anajua umuhimu wake pia.
Ø Ili kuleta mafanikio na matokeo
ya haraka Kijana ana uwezo mkubwa sana.
Ø Ni silaha nyepesi mno na hatari sana.
Ø Mungu anamtuma Yesu katika umri
wa ujana na matokeo yake ni makubwa sana.
UMUHIMU WA
KIJANA KATIKA JAMII:
a.
Kutatua
tatizo ndani ya jamii (1Samw, 17: 31-33, 46-51)
b.
Kurudisha
matumaini (Esta, 4: 12-16, 7: 1-10
c.
Kurekebisha
hali ya mambo (Mwanzo 41: 34 – 44)
d.
Kurudisha
heshima iliyopotea katika jamii.
UMUHIMU WA
KIJANA KANISANI (Math, 1: 18 – 21)
a.
Kujishughulisha
na mambo ya Kanisani kwake, kuwaza jinsi kutakavyopendeza.
b.
Kujishughulisha
na Baba yake wa Kiroho (Mchungaji) 2Tim, 1: 2 – 4.
c.
Kuomba juu
ya Kanisa / kufundisha / kuwaleta watu kwa Yesu.
d.
Kuwa mkarimu
Kanisani na nyumbani, Mf, Rebeka,Mariamu, Mwanzo 24: 13 -26.
e.
Kujitolea
kifedha,Kiakili ,Muda (Mf, Dorkasi, Warumi 12: 1)
v Kanisa lenye nguvu ni lile Vijana
wao wanajitambua.
v Kanisa lenye matokeo mazuri
linatokana na Familia zinazolijenga Kanisa.
v Kijana akikosa mwelekeo anaharibu
mwelekeo mzima wa Kanisa.
v Vijana wachache tu wanaweza
kuleta mabadiliko makubwa sana
Mf, Vijana watatu (3) Shedraki, Meshaki na Abednego (Danieli 3: 16 – 19 mst 28
-30.
v Kijana aliyebadilika moyoni mmoja
tu anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana,
Mf, Danieli 6: 24 – 28.
v Alionyesha Mungu wake na Mfalme
na jamii yote ikamwinamia Mungu wake.
v Biblia inasema mtu asiudharau
ujana wako, 1Tim, 4: 12.
v Kijana asipojitambua na
kuwajibika atadharauliwa tu kama hakuna kitu
umekifanya Kanisani kwako kinachoonekana.
v Una ulichokifanya kwa Baba yako
wa Kiroho? (Mchungaji).
v Una ulichokifanya katika jamii ya
kwenu?.
v Penda kijana ukiwepo mahali uwepo
kwa faida, usiwe hasara bali uwe faida.
v Huwezi kuheshimiwa kama hakuna kitu unachomfaidisha nacho Mungu.
v Kijana Joshua alikabidhiwa jukumu
la kuwaingiza watu Kanaani kwani alikuwa Kijana aliyejituma, aliye tayari
anayepatikana, (Hesabu, 27: 18, Kutoka, 17: 8 – 10).
MUNGU awabariki sana
By Bishop YONA P SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia.
MUNGU awabariki sana
By Bishop YONA P SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia.
No comments:
Post a Comment