Wednesday, August 28, 2013

MKIRSTO MWENYE USHAWISHI



 


{Yohana 8:31-32-Basi YESU akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, Ninyi mkikaa katika neno langu, mmekuwa wanafunzi wangu kweli kweli; tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru. }  

-lazima  uwe  mkristo  mwenye  ushawishi aliyeshiba neno la MUNGU na kweli hiyo ya MUNGU   ikikaa ndani yako hakika utakua mkristo mwenye ushawishi.

-Hatuokoki  kwenda  mbinguni  bali  tumeokoka  ili  kwenda  duniani  ili  kugusa  maisha  ya  wengine  

-ukipata  mambo haya 4 utakuwa  mkiristo  mwenye  ushawishi  

1-taarifa /information

2-ushahidi wa  kweli 

3-Maarifa /
kwenye maarifa kuna mbinu

4-kweli 

-Mtu  mwenye  taarifa  ana  nguvu 

-mkristo  mwenye  mambo  4 hayo   hapo juu  ni mkristo mwenye  ushawishi  {yohana 1:12-13 ''Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. } 
 kuna  watu  wanao fanya mambo  ya   MUNGU lakini si kimungu  


-Watu  tunaoishi  nao  wako  katika  makundi  2

-wazee  na  vijana 

-wasomi  na   wasio soma 

-matajiri  na  masikini  

-MUNGU  alipo mtumia  YESU KIRISTO  alimtuma  mtu  mwenye  taarifa  sahihi 

-{yohana 10:10b ''mimi(YESU) nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. }   {yohana 14 :6- YESU akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi. } 
ndugu  yangu hakika kupenda mambo ya MUNGU ni kupenda uzima wa milele na katika {mithali 11:27-29- BIBLIA inasema ''Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Ataabishaye nyumba yake mwenyewe ataurithi upepo; Mpumbavu atakuwa mtumwa wa mtu mwenye moyo wa akili. Mazao ya mwenye haki ni mti wa uzima; Na mwenye hekima huvuta roho za watu. } 

-Badiliko  la  tabia  hutokana  na  kujifunza 

   Ndugu hakikisha unakuwa mkristo mwenye ushawishi yaani mkristo ambaye shetani anakuogopa maana unaijua kweli ya MUNGU na hiyo kweli ambayo ni YESU KRISTO imekuweka huru mbali na dhambi na kila kusudi la shetani.
MUNGU akubariki sana .
Ni mimi ndugu yako PETER MICHAEL MABULA

                 Maisha ya ushindi.

No comments:

Post a Comment