Wednesday, August 28, 2013

JEHOVAH RAPHA (MUNGU NIKUPONYAE)


NA PETER MICHAEL MABULA

BWANA YESU asifiwe ndugu, leo tunajifunza somo linaloitwa JEHOVAH RAPHA yaani MUNGU atuponyae kama ilivyo katika Biblia kitabu cha Kutoka 15:26 katika kiebrania.
MUNGU wako lazima awe MUNGU aponyae na yeye yuko siku zote kwa ajili ya kuponya, jambo muhimu ni kwenda tu kanisani kwenye maombezi katika jina la YESU KRISTO.
[kutoka 15:26]  Biblia inasema
‘’Akawambia kwamba utaisikiza kwa biidi sauti ya BWANA MUNGU wako na  kuyafanya  yaliyoelekea  mbele  zake na kutega masikio  usikie maagizo yake na kuzishika amri  zake Mimi sitatia juu  yako  maradhi yoyote  niliyowatia wamisri; kwa kuwa  Mimi ndimi  BWANA  NIKUPONYAE ‘’  
hapo kwenye neno BWANA NIKUPONYAE  ndipo hasa kwenye kiini cha somo letu na BWANA NIKUPONYAE kwa lugha ya kiebrania ni JEHOVAH RAPHA.
ndugu zangu naomba ufahamu kwamba MUNGU hapendi kabisa kuwatesa wanadamu na magonjwa ni mashambulizi ya shetani na ndio maana kwa kusudi hilo BWANA YESU alidhihilishwa ili kuzivunja kazi za shetani (1 Yohana 3:8) na katika Maombolezo 3:33 Biblia inatuambia kuwa MUNGU hapendi kuwatesa wanadamu.
[maombolezo3:33] ‘’Maana  moyo wake hapendi  kuwatesa wanadamu  wala  kuwahuzunisha ‘’
 
-Uponyaji  hupatikana  pale MUNGU  anapoingilia kati  
  -Miujiza ni  ni  tendo  la  kimungu  ambalo liko  juu ya kanuni  za  kibinadamu [yohana3:2] 
‘’Huyu alimjia usiku akamwambia  Rabi twajua  ya kuwa  u mwalimu  umetoka  kwa MUNGU  kwa  maana  hakuna   mtu  awezaye kuzifanya  ishara  hizi  wafanyazo wewe isipokuwa  MUNGU  yu pamoja  naye  
-Maana  huyu alikuwa ametengwa yaani  najisi  au ni mtu  aliyetengwa  Mbali  na watu 

- ndugu ili upokee uponyaji lazima ujue neno la MUNGU linasemaje juu ugonjwa wako. Na uponyaji sio kupona ugonjwa tu bali hata mambo mengine ambayo unataka yapone hivyo ni muhimu kujua neno la MUNGU linasemaje juu ya ugonjwa, maovu, matendo au hata maisha yako
Mama huyu katika [marko 5:25-34] alisema ‘’nikigusa tu nitapona  yaani alichora picha moyoni  pia [marko  9:23] -ukiweza yote yanawezekana kwake yeye aminiye] maisha  yako  [isaya 53:5
‘’-Bali alijeruhiwa  kwa makosa  yetu Adhabu ya amani  yetu  ilikuwa juu  jake  na  kwa  kupigwa  kwake  sisi  tumepona’’ 
 
-Ndugu mpendwa napenda kukujulisha kwamba BWANA YESU ana nguvu sana na kwa macho yangu nimeshuhudia dada mmoja akipona UKIMWI, kaka mmoja tena ni mzee wetu wa kanisa akipona kifua kikuu(TB) na wengine wengi sana ambao wamepona magonjwa mbalimbali mengi sana na hata wewe unayeumwa hakikisha tu unaende kanisani ambapo wanamhubiri YESU na utaombewa na kupona kabisa maana hakuna ugonjwa ambao kwa YESU unashindikana. Hata kama huna neno la kujua kuhusu ugonjwa wako lakini ile imani tu ya kumwamini BWANA   ya kumwanini YESU ni neno kwani Biblia inasema katika Yohana 6:44 Kwamba ‘’ Hakuna  mtu awezaye kuja kwangu , asipovutwa na nguvu ya BABA aliyenipeleka;  nami nitamfufua siku ya mwisho.’’
-YESU ana nguvu [mathayo 8:5,13]  ‘’YESU  akawaambia  nitakuja  niponye 
KWANINI YESU ALIKUJA DUNIANI ?
Kuna vifo  vya  aina  mbili   vilikua vimetokea na sababu ya BWANA YESU kuja ili ule uhusiano wetu na MUNGU Baba yetu urudi na pia magonjwa na kila mapando ya shetani yaondolewa, tuwe wazima
1-kifo cha kimwili  yaani  mwili kutengana  na roho  
2-Roho na mwili  kutengana na MUNGU milele 
YESU alikua kurudisha haya yaani kwa njia ya kumpa YESU maisha yetu kile kilichoyutenga na MUNGU wetu hakipo tena  
-YESU anamtafuta mwenge imani  mfano  Yairo na watu  waliokuwa wanamsonga YESU katika  [Luka 17:11,19] wengine   wakaondoka  ila  mmoja  aliokoka  9 wakaondoka  baada kupona ila mmoja tu ndio akarudi hivyo ndugu hapa tunajifunza kwamba   kuokoka na miujiza ni tofauti.  Watu 9 walitendewa miujiza lakini aliyeokoka ni mmoja tu Hivyo baada ya YESU kukuponya hakikisha unadumu katika kumwabudu MUNGU pamoja na wengine katika kanisa.
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka nakuomba mpe BWANA YESU maisha yako na hiyo itakuwa ni chanzo cha uponyaji wako wa kila kitu kinachokusumbua.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

1 comment:

  1. IJUWE SIRI YA MALI NA UTAJIRI KWA NDAGU NA MAJINI PIA ASILI YAKO.

    KATIKA SAFARI YA MAFANIKIO TUNAPITIA MENGI ILI TUWEZE KUFANIKIWA LAKINI WENGI WETU KUNA MAMBO MACHACHE SANA WENGI WETU TUNAYADHARAU NA KUMBE NDIO CHANZO CHA MAFNIKIO YETU.

    N.B KWA WALE WAHITAJI WA PESA ZA NDAGU au MAJINI kwa mudamfupi nipigie DOKTA MDIRO +255 742162843

    HAYA NI MAMBO 7 YAKUZINGATIA KATIKA SAFARI YAKO YA MAFNIKIO

    i) Wazazi wako wakiwa wamekulea mpaka ukawa mkubwa wafumbua macho unawaona akikisha usiwafanye wakajuta kukuzaa asilimia kubwa wazazi wanakuwa na tabu sana ila zile tabu zao ndio zinazokufanya wewe una aminiwa na watu na unaeshimika na kujieshimu

    Kwaiyo jitahidi sana kuwa nao vizuri kuna wengi maisha yao wanaishi kwa shida chanzo ni utofauti baina ya wazazi wao

    Ukiona wazazi wako wanatabu sana usiwajibu vibaya wewe kaa nao mbali ila wape majukumu yao unacho fanya kuwaona nakurudi ulipo apo utaona mambo yako yatakuwa vizuri sana

    ii) JAMBO LA PILI
    Akikisha unatunza uzao wako yani ukijua ni mtoto ni wako basi jitahidi sana kutoa uduma ata kidogo ulicho nacho lakini udumia usiache uzao wako unateseka na njaa wewe una kula maisha aisee fahau

    Kila mtoto wako anavyo kuwa ndio mambo yako yanaaribika usipo udumia kwaiyo ukiwa waitaji kufanikiwa zaidi jali uzao wako

    iii) JAMBO LA TATU
    ukiwa umeoa au umeolewa usitoe talaka au kuomba talaka kabla mwenzio ayupo tayari kwa muda huo fahamu ukiomba talaka au akikupa talaka bila bila sababu ya msingi yeye tu ana matamanio ya kidunia basi anamuda atapoteza muelekeo wa maisha yake

    iv) UKIWA WAPATA PESA
    ukiwa wapata pesa alafu utoi sadaka basi kufikia kwenye ukuu utachelewa sana mana mana pesa badala ya kutoa kwa iyari yako utatoa kwa matatizo kwaiyo jitahidi icho icho kidogo toa sadaka kwa wenye uitaji

    v) USIMZULUMU MTU
    kama wataka kufika mbali kwenye mafanikio yako usimzulumu mtu ata kwa uchache wa kitu usifanye ivyo itakugarimu kiasi kikubwa

    vi) USIZARAH MILA
    ukiwa kwenu kuna mambo ya mila mzimu tambiko jitahidi kufatilia sana aya mambo yanarudisha nyuma sana usipo yawahi mapema

    vii)USIWE WA NAMNA
    1)ikiwa ujafanikiwa jitahidi sana usiwe mvivu kufanya kazi usiwe muhuni usiwe mwenye chuki na asira zisizo za msingi usiwe na tamaa nyoa vizuri vaa nguo za eshima na usiige maisha ya watu.

    KWA MAWSILIANO ZAIDI KUHUSU MATATIZO MBALIMBALI YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, PETE MALI ZA NDAGU NA MAJINI N.K

    DOKTA MDIRO Call/whatsup +255 742162843.

    ReplyDelete