Wednesday, August 28, 2013

NEEMA KATIKA UKOMBOZI


             







Neema katika  ukombozi maana yake mtu yoyote hawezi kabisa kuja kwa KRISTO asipovutwa kwa nguvu maalum ya MUNGU 

-Neema  ni bahati ,upendeleo au ngekewa


-Ukombozi yaani kukombolewa /kuokoka 


-Tujue kwamba tumeokolewa si kwa ujanja wetu bali ni kwa neema ya MUNGU [yohana 6;44]’’Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipo vutwa na BABA alienipeleka nami nitamfufua siku ya mwisho.’’


YESU alisema hayo kutokana na mstari wa 42 pale walipo sema huyu siye mwana wa yusufu mwana wa seremala  


Kumbe kabla ya kuamini kuna kuvutwa kwanza [wafilipi 2;13]’’Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi  lake jema’’

-Ndio maana mtu anafikia kipindi anaichukia dhambi


Tulipata neema katika ukombozi ili kutimiliza lengo lake njema [waefeso 2;8]


‘’Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha MUNGU’’ 


Neema katika ukombozi [sema neema] 

-si kwa ujanja

-si kwa nguvu zetu

-si kwa sifa zetu 

-si kwa mbwembwe zetu.  

-Bali ni kwa sababu BWANA YESU ametupenda na ametuchagua ili tupate uzima bure. Katika BIBLIA kitabu cha Yohana 15:16-17{Si ninyi mlionichagua mimi,bali ni mimi niliyewachagua ninyi:nami nikawaweka mwende mkazae matunda: na matunda yenu yapate kukaa: ili kwamba lolote  mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.’’

MUNGU HUWAVUTA WATU KWA KRISTO KWA NJIA GANI?


-Tunaposema kwamba MUNGU anawavuta watu ni rahisi kusema kwamba MUNGU anawalazmisha watu lakini hiyo sio maana yake.
Si kwamba MUNGU anamlazimisha mtu kumpa YESU maisha yake bali kwa njia ya neema yake MUNGU anaifanya hiari ya mtu ihiari yenyewe kwenda kwa YESU. Kumbuka kwa asili ya hiari ya mtu ni kujihiari yenyewe pia vile vile ni kinyume cha mapenzi ya YESU  ambaye yeye anapenda kuwa mfalme juu ya watu wanaomtii kwa hiari yao wenyewe.Zaburi 110:3’’Watu wanajitoa kwa hiari siku ya uwezo wako kwa uzuri wa utakatifu…’’
-Hiari haimlazimishwi ila inashawishika.

Njia za kuwavuta watu kwa YESU KRISTO.

1:   Roho wa MUNGU anamleta mtu kwa KRISTO hatua kwa hatua
Matendo 2:37-42(
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na BWANA MUNGU wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


(a)Hutia nuru akilini.


(b)Kuchoma dhamiri.

(c)Kumnyenyekeza mtu.

(d)Kuweka  Imani ya KRISTO ndani yake.
Biblia  hapo juu tuliposoma inasema 

-WALIPOSIKIA WAKAPATA NURU KWA SABABU YA JAMBO JEMA WALIOLISIKIA.



-Wakachomwa mioyo yao yaani WAKAJITAMBUA  KWAMBA NI WAKOSAJI.

-WAKANYENYEKEA ndio maana wakamuuliza Mtume Petro wafanyeje sasa?

- Kisha WAKAAMINI ndio maana wakabatizwa na kuokoka.

2:  Roho wa MUNGU anawavuta  watu kwa KRISTO kulingana na asili ya mwanadamu. Hosea 11:4 Biblia inasema ‘’Naliwavuta kwa kamba za kibinadamu kwa mafungo ya upendo…..’’

-Yaani anawavuta watu kwa akili zao na kutokana na asili yao.
-Anawashawishi watu kulingana na akili zao.
-Kumbuka kuwa akili za wanadamu zimepotoshwa na mambo ya dunia hivyo hatuwezi kuwashawishi watu kuokoka kwa jinsi ya kawaida tu lazima kuwaombea ili ROHO MTAKATIFU aingilie kati wakati tukiwashuhudia ukweli wa MUNGU na ukombozi pekee wa wanadamu ambao ni YESU KRISTO. 

Ndugu YESU KRISTO ni lulu yenye thamani sana. Mathayo 13:45-46(

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. 
 - Kwa wale ambao tumepata neema ya kuokolewa  ni muhimu sana kusonga mbele na pia yule ambaye bado hajatoa maisha yake kwa YESU hakika wokovu ni sasa hivyo ni muhimu kujua wakati wa neema katika ukombozi ni sasa. Maana hatujui itakavyokuwa kesho.

MUNGU awabariki sana na kwa yule ambaye hajaokoka bado nakuomba ndugu nenda katika kanisa lilalokiri wokovu na ukampe maisha yako BWANA YESU.


Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

No comments:

Post a Comment