Wednesday, August 28, 2013

KWELI SITA(6) ZA MIZIMU

Somo hili ni mwendelezo wa somo liitwalo KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO ZA MIZIMU na hii ni sehemu ya pili iitwayo


           KWELI SITA(6) ZA MIZIMU

1;
Mizimu ni malaika walioasi mbinguni

2;Mizimu  ni  wapelelezi wa shetani 

3;Mizimu inauwezo wa kutoa nyaraka au taarifa ya mtu 

4;Mizimu  inafanya kazi kupitia wafu.
 waebrania 9;27 ''Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu''
5;Mizimu  inafanya  kazi kupitia waganga  wa kienyeji 

6;Mizimu inauwezo wa kutunza taarifa za mtu, ukoo au kabila

*Kuhusu wafu mtu akifa kuna sehemu mbili tu za kwenda.

a.Paradiso –ni mahali  pa mangojeo kwa uzima  wa milele.

b.Kuzimu –ni mahali pa mangojeo pa jehanamu
Mtu akifa anatengana na wewe ukiomba mtakatifu yeyote ni kuomba mizimu, ibada za wafu ni kuabudu mizimu Luka 16:22-26{
Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.}

 Ndugu zangu hakuna mawasiliano baina ya mfu na walio hai hivyo mizimu hubeba sura ya mtu aliyekufa na sauti yake na kumtokea mtu kwa ndoto au maono au hata kumtokea moja kwa moja,
Jambo jingine la kutambua ni kwamba shetani huwafanya watu waamnini kwamba hata wao wakifa watakuja kuwatokea watu na hata wakiendelea na uovu hata wakifa wapo watu watawaombea na MUNGU atawatoa kuzimu na kuwapeleka mbinguni kitu ambacho hakipo na sio kweli. Hebu tafakari viongozi wengi wakuu wa serikali kuna siku maalumu umetengwa kwa mwaka kwamba ni siku yao na kila siku hiyo ikifika tunaenda kwenye makaburi yao na kuwaombea MUNGU awasamehe. Je wale wavuvi wanaokufa baharini na hakuna hata mmoja anayejua makaburi yao yalipo na hakuna hata mmoja anayewaombea je MUNGU siku hizi anaupendeleo? Yaani ukiwa raisi wa nchi lazima uingie pema peponi maana utakua na waombeaji wengi tena watakua na juhudi kukuombea kila mwaka siku yako ikifika jambo ambalo sio la kweli, MUNGU atusaidie na tutambue kuwa muda wa kumpa YESU maisha ni sasa wala sio baada ya kufa maana tukifa tu ni kuzimu au mbinguni na sio vinginevyo. Katika Isaya 8:19 Biblia inasema

''Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong'ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?''
Ndugu zangu pazia limekwisha kupasuka hivyo tunanaingia patakatifu moja kwa moja bila kuombewa na mtakatifu wa zamani maana BWANA YESU aliondosha kile kiambaza kilichokuwapo baina ya MUNGU na wanadamu ndiyo maana kupitia yeye(YESU) tnapata uzima bure kwa njia ya imani matendo 4:12 ''
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo''.
 ila uzima huo tunaupata tungali hai sio tukifa

MAGOJWA YANAYOSABABISHWA NA MIZIMU

Kuna magonjwa ya ukoo ya kuhama kutoka kizazi hadi kizazi na magonjwa haya husababisha na mizimu.
Pia kuna baadhi ya magonjwa yanasababishwa na mizimu mfano Pumu, kuumwa miguu, miguu kufa ganzi, vivimbe mbalimbali katika mwili, kutokukua kiroho, matumizi mabaya ya pesa  na kutokupona magonjwa. Ndugu kimbilia maombezi na utakuwa huru mbali na uonevu huu wa shetani.

Mizimu pia hutumia manabii wa uongo kwa udanganyifu au upotoshaji, mizimu pia hutumiwa na wachawi na wapandisha pepo, Mizimu pia hutumiwa na dini za uongo.

MUNGU awabariki sana 
Ni mimi ndugu yako PETER  MICHAEL
                 Maisha ya ushindiMinistry

KUFUNGULIWA KUTOKA ROHO ZA MIZIMU


Mizimu (family spirit) ni mapepo yaliyotokana na malaika walioasi pamoja na shetani ambayo watu waliyafanya kama ndugu kutoka kizazi hadi kizazi.
Mizimu no roho za shetani ambazo ni chukizo kwa MUNGU Kumbukumbu 18:9-12 ''Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, MUNGU wako usijifunze kutenda kwa mfano wa machukizo ya mataifa yale. Asionekane kwako mtu ampitishaye mwanawe au binti yake kati ya moto, wala asionekane mtu atazamaye bao, wala mtu atazamaye nyakati mbaya, wala mwenye kubashiri, wala msihiri, wala mtu alogaye kwa kupiga mafundo, wala mtu apandishaye pepo, wala mchawi, wala mtu awaombaye wafu. Kwa maana mtu atendaye hayo ni chukizo kwa BWANA; kisha ni kwa sababu ya hayo BWANA, MUNGU wako, anawafukuza mbele yako.''yanayozungumza hapo tuliposoma ni kuwahusu WAGANGA WA KIENYEJI, WACHAWI, WANAJIMU,WASIHIRI NA WANAOWAOMBA WAFU, mambo ambayo yote ni machukizo kwa MUNGU na wote hawa wanatumia mizimu kufanikisha mambo yao na kwa wale wanaomba maiti(wafu) hawa wanaomba mizimu hivyo wanahusika moja kwa moja na mizimu maana mtu aliyekufa hawezi kamwe kukusikia na hata kama anakutokea usiku tambua tu kwamba ni mizimu ambayo ni majini yanavaa sura ya ndugu yako na kuja kwako na kumbuka kuwa jini anaweza kuiga kila kitu kuanzia sauti hadi sura  na kwa sababu shetani anataka umkosee MUNGU wako kwa kumtii yeye, atakuambia mambo mengi ya kufanya, 

Yupo mama mmoja alikua anatokewa na mama yake na kumwambia kwambaCIPANGIZO 13:  GIDEAU NA ANJO YA MULUNGU  ''siku hizi umenisahau kabisa hata kaburi langu hufagii hivyo kesho asubuhi sana kafagie na unyunyuzie damu ya kuku juu ya kaburi langu.jambo hilo lilipelekee yule mama kwenda kwa mganga wa kienyeji  na
kumbuka kuwa hakuna mganga wa kienyeji asiyetumia mizimu.


akajikuta anahusika na mabo mabaya zaidi hadi kumua mtoto wake maana yule mzimu alianza kwa kutaka damu ya kuku baadae anataka kafara ya damu ya mtoto wa yule mama maana ilifika kipindi vitisho vikawa vyingi na kwa sababu mama yule alishaingia maagano na mizimu ile kwa kutii maelekezo ya kwanza akaanza kupata shinda sana na akaambiwa atapata mikosi maisha yake yote na hali hiyo ikapelekee kuua mtoto wake na cha ajabu shetani alimtumia yule mganga wa kienyeji kuongeza vitisho kwa mama na kutoa ushauri wa kumwua mtoto. Ndugu zangu jina la YESU KRISTO pekee linaloweza kuondoa mizimu maishani mwako hivyo kama unasumbuliwa na mikosi ya ukoo, mizimu ya ukoo, utasa au magonjwa ya ukoo basi kimbilia kwenye maombezi katika kanisa la kiroho karibu na wewe na utafunguliwa na kuwa salama kabisa mbali na laana zote za ukoo na mashariti ya kishetani. na katika BIBLIA kitambu cha Mambo ya walawi 19:4 inasema ''
Msigeuke kuandama sanamu, wala msijifanyizie miungu ya kusubu mimi ndimi BWANA, MUNGU wenu.''  ndugu moja ya miungu ambayo wanadamu wanaiabudu ni mizimu na kumbuka kwamba waganga wa kienyeji wanatumia mizimu katika kazi zao na ndio maana mama mmoja ambaye sasa ameokoka alikua mganga wa kienyeji zamani aliwahi kuniambia kuwa  kama mgojwa mwenye majini akija kwake kutibiwa yeye anachofanya anaongeza majini ndani ya mgojwa na kumpa mashariti ya kufanya ili abaki mzima na moja ya mashariti hayo alikua anawaambia wateja kurudi kwake kila baada ya miezi mitatu maana anajua muda wa majini kutaka ndamu umefika na kila mteja akija lazima aje na kuku mwenye rangi moja kama ni mweupe awe mweupe pote na kama ni mweusi awe mweusi pote.Katika 1 Samweli 28:7 BIBLAI inasema ''Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, Nitafutieni mwanamke mwenye pepo wa utambuzi, nipate kumwendea na kuuliza kwake. Watumishi wake wakamwambia, Tazama, yuko mwanamke mwenye pepo wa utambuzi huko Endori.'' Huyu Sauli alikua ni mfalme wa taifa la Israel ambaye aliamua kuwafuata waganga wa kienyeji na kitendo hicho kilikua ni machukizo makuu kwa MUNGU na kupelekea kunyang'anywa ufalme akapewa Daudi na huyo sauli akafa vitani na jambo lile wa kwenda kwa waganga liliongeza balaa kwa taifa badala ya kupunguza . Ndugu please please usikubali kwenda kwa waganga wa kienyeji wala usoma nyota maana watakupoteza na utakua mbali sana na MUNGU wako aliyekuumba na hakika kwa kitendo hivyo utakua unajichimbia shimo mwenyewe. ni hrei kumpelekea BWANA YESU shida zako na yeye ni mwaminifu na wa haki atakuponya na utakua huru daima maana amesema katika Mathayo 11:28 kwamba ''Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha''
MUNGU akubariki sana  wewe usiye na mizimu maishani mwako maana ulimpa BWANA YESU maisha yako na ukatengwa mbali na mizimu ya ukoo ambao ipo katika kila mtu ambaye hajasafishwa kwa damu ya YESU maana mizimu hiyo ipo tangu kizazi na kizazi na mambo mengi yanawapata ukoo fulani fulani tu kwa sababu ya mizimu, ukielewa hivyo chukua hatua kwa kumpa YESU maisha yako na utakua huru pia utakua ufunguo katika ukoo wetu kuwafukuza mizimu ya mababu ambayo imeleta balaa kubwa katika maisha. maana wapo watu wao wanajifahamu ni watu wasio na akili shuleni yaani ukoo mzima hakuna anayeweza kufauli kwenda sekondari na hawajui tatizo ni nini lakini kumbe tatizo ni mizimu ya ukoo.
MUNGU akubariki na  somo litaendelea kwa kuangalia mambo 6 kuhusu mizimu.

 ni mimi ndugu yako PETER MICHAEL wa maisha ya ushindi

NDOTO NA MAONO.

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye
New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.


Kama ilivyoandikwa katika (Matendo ya Mitume 2:17)”Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu ,nitawamwagia watu Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto”. LEO TUTAJIFUNZA JUU YA NDOTO NA MAONO.

Dhana ya Ndoto.
Ni picha zinazoambatana na sauti kama sinema ambazo mtu huziona anapokuwa amesinzia. (Mwanzo 28:10-15).
Maono- ni picha ambazo mtu huziona anapokuwa macho yaani akiwa hajasinzia.
Tofauti iliyopo baina ya hivi vitu viwili ni kuwa, kimoja hutokea usingizini wakati kingine hutokea katika hali ya kawaida pasipo kuwa usingizini.
Sifa kuu ya Ndoto na Maono ni kuwa ni Mafumbo. Hii ina maana kwamba, mawasiliano haya ya kiroho huja kwa namna isiyo ya kawaida, hivyo hayawi na tafsiri ya moja kwa moja. (Hesabu 12 :5-8). Aidha, hakuna kanuni maalumu katika kutafta tafsiri zake (Mwanzo 37 :5-7), japo watu wa Mungu wanaweza kufunuliwa maana ya ndoto, kumbuka Yusufu alivyotafsi ndoto akiwa gerezan. izingatiwe kuwa wakati mwingine, ndoto zaidi ya moja,zinaweza kumaanisha kitu kimoja (Mwanzo 41 :1-7,14-16,25-38)
Mfano: Kornelio aliona maono saa tisa mchana (Matendo 10:1-6)
Petro aliona maono saa sita mchana (Matendo 10:9-16)
Paulo aliona maono alipokuwa njiani kwenda Dameski ilikuwa adhuhuri (Matendo 26:12-16)
Musa alipewa maono alipokuwa akichunga kondoo wa mkwewe Yethro mchana (Kutoka 3:1-3)
Hata hivyo, kuota si kwa watu waliookoka tu, bali hata ambao hawajaokoka wanawezakuota ndoto na kuona maono ya kimungu.
Mfano wa watu ambao hawakuwa wacha Mungu lakini waliweza kuota na kuona maono ya kimungu ni kama ifuatavyo:
Farao (Mwanzo 41:1)
Nebukadreza (Daniel 4:4-5)
Mkewe Pilato Mathayo (27:17-19)
Kornelio (Matendo 10:1-4).
Kutokana na Mifano hiyo hapo juu tunaona kuwa,mtu yeyote anaweza kuota na kuona maono ya kimungu.
Tatizo ni namna ya kupata maarifa ya kupambanua au kutafsiri ndoto hiyo au maono hayo. Hapa inatokana na kuwa ndoto au maono hayana jibu moja, na wala si kila ndoto inatoka kwa Mungu. Na hapa ndipo Hosea anapoliasa kanisa juu ya kuwa na maarifa (Hosea 4:6).
AINA ZA NDOTO.
Aina ya ndoto hutegemea chanzo chake.
VYANZO VYA NDOTO NA MAONO.
Kuna vyanzo vikuu vitatu vya ndoto/maono.
(i) Ndoto au maono yatokanayo na nafsi ya mtu mwenyewe.
Hii hutokana na shughuli alizokuwa akizifanya kutwa nzima,hivyo anapoenda kulala,matukio ya siku nzima hujirudia kutokana na picha zilizohifadhiwa katika ubongo wake. (Mhubiri 5:3)
Kwamaana ndoto huja kwasababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya maneno.
Vilevile, mtu anapotafakari kitu kwa muda mrefu. (Isaya 29:8)
Tena itakuwa kama mtu mwenye njaa aotapo, kumbe anakula ; lakini aamkapo,nafsi yake haina kitu…
(ii) Ndoto au maono yanayotoka kwa shetani.
Ndoto hizi,huambatana na vitisho,hutuondolea amani, kuogofya na kutuacha katika hali ya taharuki ya woga. Ndoto hizi huchosha mwili na akili. (Ayubu 7 :14) Biblia inasema « ndipo unitishapo kwa ndoto,na kunitia hofu kwa maono ».
Hizi ndoto hazitoki kwa Mungu kwa kuwa Mungu kamwe hawezi kutupa ndoto za namna hii (2Timotheo 1 :7) « Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi »

MAKUSUDI YAKE NI NINI ?


Kutupoteza na kutupeleka mbali na neno la Mungu.

(Zaburi 119 :95,Ufunuo2 :20 1Yohana2 :26)
Kutuonea. (Matendo 10 :38)
Kututesa. (1Petro 5:8-9)
Kutushambulia kwa kutumia sura za kutisha. (Ayubu 16:14).
Kuitichafua miili yetu kupitia ndoto za uasherati na uzinzi na mapepo au watu/mizimu Yuda (1:6-8)
Kututisha na kutupa hofu ili tusiendelee.(Ayubu 7:13-15)

(iii) Ndoto au Maono Yanayotoka Kwa Mungu.(Mwanzo 20:3,Kutoka 3:2)

Tofauti ya zile za Shetani, hizi huambatana na amani ya Mungu!hii ni kwa kuwa Mungu ni wa amani wala si wa machafuko. Hivyo, ndoto yoyote unayoona inaleta machafuko,ujue si ya Mungu.

MAKUSUDI YA NDOTO HIZI NI YAPI ?


Mungu, hutumia njia hii kuwasiliana na watu wake. Mawasiliano haya huwa na shabaha anuwai (Ayubu 33 :14-15) kama ifuatavyo :

Kutupa maelekezo (Mathayo 2:13, Matendo 9 :10-12,Mwanzo 20 :3-7)
Kutuonya/Kututahadharisha juu ua hatari (Matahyo 2:12, Mwanzo 31:24)
Kufanya mawasiliano nasi na kutueleza au kutulewesha mambo mbalimbali Mwanzo 28:10-16,1Wafalme 3:5-15)
Kutuondolea mashaka na wasiwasi juu ya jambo ie kutuongoza palipo sahihi.
(Mathayo 1:20,Matendo 16:6-10)
Kumshughulikia mtu ili kuubadiri mwelekeo wake usio sahihi pengine. (Mathayo 27:19)
Hutuonyesha mambo tusiyoyajua kwaajili ya kanisa au sisi binafsi (Ufunuo 1:1)

Namna ya Kupata tafsiri ya Ndoto au Maono yatokanayo na Mungu.

Kama nilivyotangulia kusema, hakuna kanuni maalum wala taaluma inayohusiana na vitu hivi, hivyo kwa kutumia mawazo yetu au hekima zetu wenyewe si rahisi kupata tafsiri sahihi. Tutajidanganya wenyewe na hapo ndipo tunapopaswa kukumbuka (Mwanzo 40:8) Wakamwambia, tumeota ndoto wala hapana awezaye kufasiri.Yusufu akawaambia, kufasiri ndoto si kazi ya Mungu?Tafadhari mniambie.
HATUA KATIKA KUPATA MAJIBU YA NDOTO/MAONO.
1. Mara tu, baada ya maono au ndoto kuisha, muda ule ule, unapaswa kutulia kimya na kutafakairi kwa muda, na hapo ndipo roho wa Mungu anapoweza kutupa maelezo ya maono/ndoto hiyo (Matendo 10:9-20).izingatiwe kuwa si lazima Mungu afanye hivyo kwa muda huo, hivyo endapo hatafanya hivyo, ni vema sasa ufuate hatua ya pili ambayo ni hii ifuatayo.

2. Kumwomba Mungu tafsiri moja kwa moja.

Baada ya kutulia kwa muda,kama hujapata tafsiri, tunapaswa kumwomba Mungu mwenyewe atafsiri (Daniel 2:16-19). Na endapo hatujapata majibu bado, tunapaswa kulala na hata kuisahau ndoto hiyo,hapo Mungu huweza kukuletea ndoto ile ile tena huku akiifafanua kwa namna flani. Anaweza kuleta moja au hata zaidi. Tunapaswa kuwa na subira pia (Mwanzo 41:17-23) kwani pengine, anawezaa kukukumbusha juu ya matukio utakayo yaona katika maisha yako siku zitakazofuata. (Waamuzi 7:7-15)
3. Kuuliza Katika Maono au Ndoto.
Hatua hii, hutumika mara unapokuwa unapewa maono moja kwa moja kutoka kwa wale watu au viumbe wanaokuwa wanakupa ujumbe huo. Mara zote, kiumbe yeyote atakaye kuja kwako, atajitambulisha kuwa yeye ni nani na ametumwa na nani kwako, kisha ndiyo atatoa ujumbe aliotumwa kwako. Kama ni malaika wa Mungu, kwanza atakusalimia kwa salamu ya Usiogope na hapa utajisikia amani sana moyoni mwako (Daniel 10 :19, Luka 1 :13, 30) na endapo utaendela kuogopa kemea kwa jina la Yesu, huyo hatakuwa Malaika. Matokeo ya kukemea yatakuthihirishia kuwa huyo ni nani.
Angalizo ; malaika yeyote atakayetumwa kwako atakapojitambulisha, atakachokwambia utapaswa kukipima kulingana na neno la Mungu. Mfano, akikwambia umechanguliwa kuliko wanawake wote duniani kuwa utamzaa masihi wa Bwana.Lazima ujue kuwa hiyo si kweli, kwani masihi alisha kuzaliwa miaka zaidi ya 2000 iliyopita.

Izingatiwe kuwa, Mungu huweza kutuma ujumbe kwako kupitia malaika wake au watu walio hai wala si watu waliokufa kama vile mitume n.k. mfano, ukisikia mtu anajitambulisha kwako akikwambia kuwa yeye ni Paulo,Ayubu,Bikra Mariam n.k. ujue huo ni ujanja wa shetani anataka akutapeli kwa kukudanganya.

Tahadhari : wakati mwingine unaweza ukatokewa na kiumbe atakayejitambulisha kwako kama « Malkia wa Mbingu » huyu kiumbe alikuwepo tangu enzi zile za nabii Yeremia huko Misri (Yeremia 6 :18 )na kwa kuwa hujitambulisha kama mtakatifu, bais amewapoteza watu wengi wa Mungu kwa kutolijua neno hili. (Yeremia 44 :17-19,25).
Kiumbe huyu ndiye aliye watokea watoto wa Fatma yaani Lusia, Franscis na Yasinta akijitambulisha kuwa yeye ni Bikra Maria na kuwafundisha wasali rozali. Izingatiwe kuwa Yesu, alisha tufundisha namna ya kuomba, kuwa ni kupitia jina lake tu, pia akasema kuwa yeye ni mwanzo na mwisho (Ufunuo 22 :13) hivyo, hatutegemei kusikia mtu mwingine atakaekuja kwa lolote badala yake. Lakujihadhari sana ni kuwa, pepo huyu anauwezo wa kufanya miujiza kama ya Yesu, hivyo ni lazima kuwa makini ili asije akaliteka kanisa.

4. Kutosumbuka tusipopata tafsiri ya Ndoto.

Kama Mungu ametuma ndoto kwako, hakika atakupa na tafsiri yake. Endapo utazingatia vigezo vyote hapo juu bado usipate majibu tulia, Mungu mwenyewe atashughulika na tafsiri ya ndoto hiyo.(Luka 12 :25-26). Hii inatokana na kwamba, ndoto hii inaweza ikawa imetokana na nafsi zetu wenyewe, au shetani au pengine ikawa ni ya muda mrefu sana ujao, hivyo tafsiri yake si ya lazima kwasasa. Lamsingi, tunapaswa kutunza kil akitu kwenye kumbukumbu sahihi. (Habakuki 2 :2-3, Daniel 10 :14)
HITIMISHO.
Tunapaswa kuzipinga ndoto na maono ya kufarakanisha kwani hazitoki kwa Mungu hizo. Shetani ni mfitini, hutumia ndoto na maono ili kutugombanisha. Hapendi aone upendo, amani na ushirikiano baina yetu,hivyo huchukua mwanya wa maono na ndoto kuonesha madhaifu ya wenzetu ili tudhoofishane, tusiaminiane. Tuwaone wenzetu watenda maovu kama vile wachawi,wazinzi,n.k. ili kupanda mbegu ya chuki miongoni mwetu. Ndoto kama hizi tunapaswa kuzitupilia mbali kwani ni za baba wa uongo si za Mungu.Kamwe Mungu hawezi kutuonyesha ubaya wa wengine bali hutuonyesha ubaya wetu wenyewe ili tuweze kutubu (Mithali 6 :16, Yakobo 3 :15-17 ;Daniel 5 :1-6).

Mwl Sospeter Simon S. Ndabagoye

New Elshaddai Ministries NEM-Tanzania.

NAOTA NDOTO NYEVU JE NI DHAMBI AU SIO DHAMBI?

 NA PETER MICHAEL MABULA ''NENO LA MUNGU NI SILAHA TOSHA KUANGAMIZA KAZI ZA SHETANI MAISHANI MWETU

shikamoo!! natumai u mzima wa afya, please naomba ushauri wako ni kwamba mara nyingi sana mtu unapofikia ule umri wa utu uzima yaani kuanzia miaka 14 na kuendelea uwa vijana tunapata ndoto nyevu(yaan unaota uko na msichana flani mnafanya tendo la ndoa) na unapozinduka ndoton unakuta kweli umechafuka )yaani kama umefikia mshndo) na kidini haturusiwi kuzini mpaka tutakapofunga ndoa je hii haiwezi kuwa ni mojawapo ya kuzini na ikawa inafaa kutibiwa?? na tufanyeje kuepukana nazo hizo ndoto maana inakuwa kama picha halisi?? MAJIBU


nashukuru sana ndugu kwa kunieleza jambo hilo kiukweli ni wachache sana wanaoweza kuomba ushauri kwa mambo kama hayo hivyo hongera sana mtu wa MUNGU. kuhusu swali lako ni kweli ndoto hizi hutokea sana kwa vijana wa kiume na wa kike na ukweli ni kwamba ndoto hizi zimegawanyika katika sehemu mbili {1]vitu vya uzazi mfano shahawa lazima zitoke kama zimezidi hivyo upo utaratibu wa kuviondoa mfano kamasi ikimaliza kazi yake hutoka au tongotongo lazima zitoke na mchakato huu wakati mwingine hutoka kwa njia ya ndoto na mfano kwa wanawake kwa mwezi lazima kuna uchafu unatoka baada ya yai kungoja mbegu ya kiume na kufikia hali ya kuharibika hivyo lazima yai lipasuke na kuwa uchafu na uchafu huo lazima utoke na kwa mwanaume ni hivyo shahawa zinapoongezeka sana inafikia mahali zinatoka na kwa maumbile ya mwanaume wakati mwingine hutoka kwa njia ya ndoto. wapendwa wengi hutaka kila jambo liwe la kiroho lakini mengine sio ya kiroho. [2] pia shetani naye hutaka kuharibu watu au kuwateka watu hivyo kwa sababu uasherati/uzinzi ni moja ya dhambi zinazoongoza kutendwa na wanadamu naye hutaka kutumia njia hiyo kuwanasa vijana mfano zamani kidogo kama miaka 8 imepita kipindi hicho nilikua na miaka 19 niliota nafanya mapenzi na dada mmoja na na shahawa zikatoka nyingi sana hadi kero na kesho yake nikamweleza rafiki yangu mmoja ushauri alionipa aliniambia nitafute msichana au nipige punyeto na mimi sikutafuta msichana ila nilipiga punyeto sana lakini na usiku nikaota tena sasa kama tatizo lilikuwa kutaka kupunguzwa shahawa je kwanini nimeota tena wakati shahawa zimeshatoka nyingi kiasi hicho kwa hiyo ndugu hiyo ilikuwa ujanja wa shetani aninase na alininasa maana nilitenda dhambi ya kupiga punyeto na mimi nilikua naota sana hizo ndoto hadi nilipookoka ndipo zilikoma na nikajua huyu alikua ni shetani kutaka kuninasa na alininasa kwa miaka mingi sana.Nilipookoka nilikaa zaidi ya miezi 10 bila kuota ndoto hizo na mwezi huo wa 10 nikaota kiukweli nilifunga siku mbili maombi ili kuua roho hiyo iliyonirudia lakini haikuwa roho kunirudia ila ilikuwa ni njia tu ya kuondoa uchafu uliozidi mwilini na baada ya hapo nilikaa tena kama miezi 5 nikaota tena hivyo kwa miaka kama 4 nimeota nadhani haivuki mara 6 na sikutenda dhambi kwa sababu ya hilo jambo. Hivyo ndugu hizo ndoto kama zinakutokea kwa wingi sana jua ya kwamba ni shetani hivyo mshirikishe mchungaji na wewe mwenyewe omba na hali hiyo itakoma maana hata mimi nilijishangaa sana nikawaza kila siku nakemea mapepo na yanatoka nimeombea watu wengi na MUNGU amewaponya sasa iweje jambo hili ina maana MUNGU hakunilinda na hili lakini ndio hivyo ni njia tu ya kuondoa shahawa zilizozidi lakini isiwe kila siku mimi naamini lazime iwe baada ya muda mrefu na pia kama ikikutokea jitahidi usitende dhambi maana shetani anaweza kuwatumia rafiki zako ambao wataliona tukio au utataka ushauri kwao maana zipo njia nyingi za shetani kutaka kuwanasa wateule wa MUNGU. la mwisho kama hujampatia YESU KRISTO maisha yako jua ya kuwa wachawi au majini wanaweza kukufanya wanavyotaka mfano wadada wengi nimeshiriki kuwaombea kanisani kwetu ambao walikuwa wanaingiliwa na majini kila siku na wakati anaingiliwa anajiona kama yuko dunia nyingine kumbe shetani na hila zake pia wakaka wengi wamekuwa wanafanya mapenzi na majini na haya yote wakati mwingine mhusika hudhani ni ndoto kumbe ni majini na ni tukio halisi. lakini kama umeokoka na uko vizuri kwa MUNGU wako hakuna jini wala mchawi atakayekugusa na mimi naamini shetani yuko kazini maana hata mimi kabla sijaokoka nilikuwa naota sana hizo ndoto yaani hata mara 2 kwa wiki lakini nilipookoka haikuwa hivyo na nikajua kabisa alikuwa ni shetani na malaika zake. MUNGU akubariki sana na kama una swali jingine uliza tu na kwa kile ninachofahamu nitakuambia.

JEHOVAH RAPHA (MUNGU NIKUPONYAE)


NA PETER MICHAEL MABULA

BWANA YESU asifiwe ndugu, leo tunajifunza somo linaloitwa JEHOVAH RAPHA yaani MUNGU atuponyae kama ilivyo katika Biblia kitabu cha Kutoka 15:26 katika kiebrania.
MUNGU wako lazima awe MUNGU aponyae na yeye yuko siku zote kwa ajili ya kuponya, jambo muhimu ni kwenda tu kanisani kwenye maombezi katika jina la YESU KRISTO.
[kutoka 15:26]  Biblia inasema
‘’Akawambia kwamba utaisikiza kwa biidi sauti ya BWANA MUNGU wako na  kuyafanya  yaliyoelekea  mbele  zake na kutega masikio  usikie maagizo yake na kuzishika amri  zake Mimi sitatia juu  yako  maradhi yoyote  niliyowatia wamisri; kwa kuwa  Mimi ndimi  BWANA  NIKUPONYAE ‘’  
hapo kwenye neno BWANA NIKUPONYAE  ndipo hasa kwenye kiini cha somo letu na BWANA NIKUPONYAE kwa lugha ya kiebrania ni JEHOVAH RAPHA.
ndugu zangu naomba ufahamu kwamba MUNGU hapendi kabisa kuwatesa wanadamu na magonjwa ni mashambulizi ya shetani na ndio maana kwa kusudi hilo BWANA YESU alidhihilishwa ili kuzivunja kazi za shetani (1 Yohana 3:8) na katika Maombolezo 3:33 Biblia inatuambia kuwa MUNGU hapendi kuwatesa wanadamu.
[maombolezo3:33] ‘’Maana  moyo wake hapendi  kuwatesa wanadamu  wala  kuwahuzunisha ‘’
 
-Uponyaji  hupatikana  pale MUNGU  anapoingilia kati  
  -Miujiza ni  ni  tendo  la  kimungu  ambalo liko  juu ya kanuni  za  kibinadamu [yohana3:2] 
‘’Huyu alimjia usiku akamwambia  Rabi twajua  ya kuwa  u mwalimu  umetoka  kwa MUNGU  kwa  maana  hakuna   mtu  awezaye kuzifanya  ishara  hizi  wafanyazo wewe isipokuwa  MUNGU  yu pamoja  naye  
-Maana  huyu alikuwa ametengwa yaani  najisi  au ni mtu  aliyetengwa  Mbali  na watu 

- ndugu ili upokee uponyaji lazima ujue neno la MUNGU linasemaje juu ugonjwa wako. Na uponyaji sio kupona ugonjwa tu bali hata mambo mengine ambayo unataka yapone hivyo ni muhimu kujua neno la MUNGU linasemaje juu ya ugonjwa, maovu, matendo au hata maisha yako
Mama huyu katika [marko 5:25-34] alisema ‘’nikigusa tu nitapona  yaani alichora picha moyoni  pia [marko  9:23] -ukiweza yote yanawezekana kwake yeye aminiye] maisha  yako  [isaya 53:5
‘’-Bali alijeruhiwa  kwa makosa  yetu Adhabu ya amani  yetu  ilikuwa juu  jake  na  kwa  kupigwa  kwake  sisi  tumepona’’ 
 
-Ndugu mpendwa napenda kukujulisha kwamba BWANA YESU ana nguvu sana na kwa macho yangu nimeshuhudia dada mmoja akipona UKIMWI, kaka mmoja tena ni mzee wetu wa kanisa akipona kifua kikuu(TB) na wengine wengi sana ambao wamepona magonjwa mbalimbali mengi sana na hata wewe unayeumwa hakikisha tu unaende kanisani ambapo wanamhubiri YESU na utaombewa na kupona kabisa maana hakuna ugonjwa ambao kwa YESU unashindikana. Hata kama huna neno la kujua kuhusu ugonjwa wako lakini ile imani tu ya kumwamini BWANA   ya kumwanini YESU ni neno kwani Biblia inasema katika Yohana 6:44 Kwamba ‘’ Hakuna  mtu awezaye kuja kwangu , asipovutwa na nguvu ya BABA aliyenipeleka;  nami nitamfufua siku ya mwisho.’’
-YESU ana nguvu [mathayo 8:5,13]  ‘’YESU  akawaambia  nitakuja  niponye 
KWANINI YESU ALIKUJA DUNIANI ?
Kuna vifo  vya  aina  mbili   vilikua vimetokea na sababu ya BWANA YESU kuja ili ule uhusiano wetu na MUNGU Baba yetu urudi na pia magonjwa na kila mapando ya shetani yaondolewa, tuwe wazima
1-kifo cha kimwili  yaani  mwili kutengana  na roho  
2-Roho na mwili  kutengana na MUNGU milele 
YESU alikua kurudisha haya yaani kwa njia ya kumpa YESU maisha yetu kile kilichoyutenga na MUNGU wetu hakipo tena  
-YESU anamtafuta mwenge imani  mfano  Yairo na watu  waliokuwa wanamsonga YESU katika  [Luka 17:11,19] wengine   wakaondoka  ila  mmoja  aliokoka  9 wakaondoka  baada kupona ila mmoja tu ndio akarudi hivyo ndugu hapa tunajifunza kwamba   kuokoka na miujiza ni tofauti.  Watu 9 walitendewa miujiza lakini aliyeokoka ni mmoja tu Hivyo baada ya YESU kukuponya hakikisha unadumu katika kumwabudu MUNGU pamoja na wengine katika kanisa.
MUNGU akubariki sana na kama hujaokoka nakuomba mpe BWANA YESU maisha yako na hiyo itakuwa ni chanzo cha uponyaji wako wa kila kitu kinachokusumbua.
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

NEEMA KATIKA UKOMBOZI


             







Neema katika  ukombozi maana yake mtu yoyote hawezi kabisa kuja kwa KRISTO asipovutwa kwa nguvu maalum ya MUNGU 

-Neema  ni bahati ,upendeleo au ngekewa


-Ukombozi yaani kukombolewa /kuokoka 


-Tujue kwamba tumeokolewa si kwa ujanja wetu bali ni kwa neema ya MUNGU [yohana 6;44]’’Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipo vutwa na BABA alienipeleka nami nitamfufua siku ya mwisho.’’


YESU alisema hayo kutokana na mstari wa 42 pale walipo sema huyu siye mwana wa yusufu mwana wa seremala  


Kumbe kabla ya kuamini kuna kuvutwa kwanza [wafilipi 2;13]’’Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi  lake jema’’

-Ndio maana mtu anafikia kipindi anaichukia dhambi


Tulipata neema katika ukombozi ili kutimiliza lengo lake njema [waefeso 2;8]


‘’Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha MUNGU’’ 


Neema katika ukombozi [sema neema] 

-si kwa ujanja

-si kwa nguvu zetu

-si kwa sifa zetu 

-si kwa mbwembwe zetu.  

-Bali ni kwa sababu BWANA YESU ametupenda na ametuchagua ili tupate uzima bure. Katika BIBLIA kitabu cha Yohana 15:16-17{Si ninyi mlionichagua mimi,bali ni mimi niliyewachagua ninyi:nami nikawaweka mwende mkazae matunda: na matunda yenu yapate kukaa: ili kwamba lolote  mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.’’

MUNGU HUWAVUTA WATU KWA KRISTO KWA NJIA GANI?


-Tunaposema kwamba MUNGU anawavuta watu ni rahisi kusema kwamba MUNGU anawalazmisha watu lakini hiyo sio maana yake.
Si kwamba MUNGU anamlazimisha mtu kumpa YESU maisha yake bali kwa njia ya neema yake MUNGU anaifanya hiari ya mtu ihiari yenyewe kwenda kwa YESU. Kumbuka kwa asili ya hiari ya mtu ni kujihiari yenyewe pia vile vile ni kinyume cha mapenzi ya YESU  ambaye yeye anapenda kuwa mfalme juu ya watu wanaomtii kwa hiari yao wenyewe.Zaburi 110:3’’Watu wanajitoa kwa hiari siku ya uwezo wako kwa uzuri wa utakatifu…’’
-Hiari haimlazimishwi ila inashawishika.

Njia za kuwavuta watu kwa YESU KRISTO.

1:   Roho wa MUNGU anamleta mtu kwa KRISTO hatua kwa hatua
Matendo 2:37-42(
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na BWANA MUNGU wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


(a)Hutia nuru akilini.


(b)Kuchoma dhamiri.

(c)Kumnyenyekeza mtu.

(d)Kuweka  Imani ya KRISTO ndani yake.
Biblia  hapo juu tuliposoma inasema 

-WALIPOSIKIA WAKAPATA NURU KWA SABABU YA JAMBO JEMA WALIOLISIKIA.



-Wakachomwa mioyo yao yaani WAKAJITAMBUA  KWAMBA NI WAKOSAJI.

-WAKANYENYEKEA ndio maana wakamuuliza Mtume Petro wafanyeje sasa?

- Kisha WAKAAMINI ndio maana wakabatizwa na kuokoka.

2:  Roho wa MUNGU anawavuta  watu kwa KRISTO kulingana na asili ya mwanadamu. Hosea 11:4 Biblia inasema ‘’Naliwavuta kwa kamba za kibinadamu kwa mafungo ya upendo…..’’

-Yaani anawavuta watu kwa akili zao na kutokana na asili yao.
-Anawashawishi watu kulingana na akili zao.
-Kumbuka kuwa akili za wanadamu zimepotoshwa na mambo ya dunia hivyo hatuwezi kuwashawishi watu kuokoka kwa jinsi ya kawaida tu lazima kuwaombea ili ROHO MTAKATIFU aingilie kati wakati tukiwashuhudia ukweli wa MUNGU na ukombozi pekee wa wanadamu ambao ni YESU KRISTO. 

Ndugu YESU KRISTO ni lulu yenye thamani sana. Mathayo 13:45-46(

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. 
 - Kwa wale ambao tumepata neema ya kuokolewa  ni muhimu sana kusonga mbele na pia yule ambaye bado hajatoa maisha yake kwa YESU hakika wokovu ni sasa hivyo ni muhimu kujua wakati wa neema katika ukombozi ni sasa. Maana hatujui itakavyokuwa kesho.

MUNGU awabariki sana na kwa yule ambaye hajaokoka bado nakuomba ndugu nenda katika kanisa lilalokiri wokovu na ukampe maisha yako BWANA YESU.


Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

NEEMA KATIKA UKOMBOZI


             







Neema katika  ukombozi maana yake mtu yoyote hawezi kabisa kuja kwa KRISTO asipovutwa kwa nguvu maalum ya MUNGU 

-Neema  ni bahati ,upendeleo au ngekewa


-Ukombozi yaani kukombolewa /kuokoka 


-Tujue kwamba tumeokolewa si kwa ujanja wetu bali ni kwa neema ya MUNGU [yohana 6;44]’’Hakuna mtu awezaye kuja kwangu asipo vutwa na BABA alienipeleka nami nitamfufua siku ya mwisho.’’


YESU alisema hayo kutokana na mstari wa 42 pale walipo sema huyu siye mwana wa yusufu mwana wa seremala  


Kumbe kabla ya kuamini kuna kuvutwa kwanza [wafilipi 2;13]’’Kwa maana ndiye MUNGU atendaye kazi ndani yenu kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi  lake jema’’

-Ndio maana mtu anafikia kipindi anaichukia dhambi


Tulipata neema katika ukombozi ili kutimiliza lengo lake njema [waefeso 2;8]


‘’Kwa maana mmeokolewa kwa neema kwa njia ya imani ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu ni kipawa cha MUNGU’’ 


Neema katika ukombozi [sema neema] 

-si kwa ujanja

-si kwa nguvu zetu

-si kwa sifa zetu 

-si kwa mbwembwe zetu.  

-Bali ni kwa sababu BWANA YESU ametupenda na ametuchagua ili tupate uzima bure. Katika BIBLIA kitabu cha Yohana 15:16-17{Si ninyi mlionichagua mimi,bali ni mimi niliyewachagua ninyi:nami nikawaweka mwende mkazae matunda: na matunda yenu yapate kukaa: ili kwamba lolote  mmwombalo BABA kwa jina langu awapeni.’’

MUNGU HUWAVUTA WATU KWA KRISTO KWA NJIA GANI?


-Tunaposema kwamba MUNGU anawavuta watu ni rahisi kusema kwamba MUNGU anawalazmisha watu lakini hiyo sio maana yake.
Si kwamba MUNGU anamlazimisha mtu kumpa YESU maisha yake bali kwa njia ya neema yake MUNGU anaifanya hiari ya mtu ihiari yenyewe kwenda kwa YESU. Kumbuka kwa asili ya hiari ya mtu ni kujihiari yenyewe pia vile vile ni kinyume cha mapenzi ya YESU  ambaye yeye anapenda kuwa mfalme juu ya watu wanaomtii kwa hiari yao wenyewe.Zaburi 110:3’’Watu wanajitoa kwa hiari siku ya uwezo wako kwa uzuri wa utakatifu…’’
-Hiari haimlazimishwi ila inashawishika.

Njia za kuwavuta watu kwa YESU KRISTO.

1:   Roho wa MUNGU anamleta mtu kwa KRISTO hatua kwa hatua
Matendo 2:37-42(
Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake YESU KRISTO, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha ROHO MTAKATIFU. Kwa kuwa ahadi hii ni kwa ajili yenu, na kwa watoto wenu, na kwa watu wote walio mbali, na kwa wote watakaoitwa na BWANA MUNGU wetu wamjie. Akawashuhudia kwa maneno mengine mengi sana na kuwaonya, akisema, Jiokoeni na kizazi hiki chenye ukaidi. Nao waliolipokea neno lake wakabatizwa; na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu.  Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali.


(a)Hutia nuru akilini.


(b)Kuchoma dhamiri.

(c)Kumnyenyekeza mtu.

(d)Kuweka  Imani ya KRISTO ndani yake.
Biblia  hapo juu tuliposoma inasema 

-WALIPOSIKIA WAKAPATA NURU KWA SABABU YA JAMBO JEMA WALIOLISIKIA.



-Wakachomwa mioyo yao yaani WAKAJITAMBUA  KWAMBA NI WAKOSAJI.

-WAKANYENYEKEA ndio maana wakamuuliza Mtume Petro wafanyeje sasa?

- Kisha WAKAAMINI ndio maana wakabatizwa na kuokoka.

2:  Roho wa MUNGU anawavuta  watu kwa KRISTO kulingana na asili ya mwanadamu. Hosea 11:4 Biblia inasema ‘’Naliwavuta kwa kamba za kibinadamu kwa mafungo ya upendo…..’’

-Yaani anawavuta watu kwa akili zao na kutokana na asili yao.
-Anawashawishi watu kulingana na akili zao.
-Kumbuka kuwa akili za wanadamu zimepotoshwa na mambo ya dunia hivyo hatuwezi kuwashawishi watu kuokoka kwa jinsi ya kawaida tu lazima kuwaombea ili ROHO MTAKATIFU aingilie kati wakati tukiwashuhudia ukweli wa MUNGU na ukombozi pekee wa wanadamu ambao ni YESU KRISTO. 

Ndugu YESU KRISTO ni lulu yenye thamani sana. Mathayo 13:45-46(

Tena ufalme wa mbinguni umefanana na mfanya biashara, mwenye kutafuta lulu nzuri; naye alipoona lulu moja ya thamani kubwa, alikwenda akauza alivyo navyo vyote, akainunua. 
 - Kwa wale ambao tumepata neema ya kuokolewa  ni muhimu sana kusonga mbele na pia yule ambaye bado hajatoa maisha yake kwa YESU hakika wokovu ni sasa hivyo ni muhimu kujua wakati wa neema katika ukombozi ni sasa. Maana hatujui itakavyokuwa kesho.

MUNGU awabariki sana na kwa yule ambaye hajaokoka bado nakuomba ndugu nenda katika kanisa lilalokiri wokovu na ukampe maisha yako BWANA YESU.


Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula

KUOKOKA NI NINI?



              


Watu wengi wamekua wakijiuliza kuhusu kuokoka ni nini, jamii nyingine wamekua wakipinga jambo la kuokoka hapa duniani kana kwamba wataweza kutenda jambo wakiwa marehemu ambalo litawafanya waokoke.  Lakini kuokoka wanadamu tunaokoka hapa hapa duniani  maana hatuwezi kufanya chochote tukiwa wafu hivyo kwa maamuzi ya leo unaweza kuokoka, kwa matendo yako ya sasa unaweza kuokoka na sio baadae baada ya kufa.

*Kuokoka ni kumwamini YESU KRISTO.Yohana 1:12 -13‘’Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa MUNGU, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa MUNGU. ‘’
Kumwamini YESU ni kumkubali YESU na pia kumtegemea kwa kila kitu, na yeye alisema kwamba sisi bila yeye hatuwezi kufanya lolote hata lile lililo dogo kabisa.
Matendo 16:30-31 Biblia inasema ‘’
kisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, yanipasa nifanye nini nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini BWANA YESU, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako. ‘’

*Tukimwamini BWANA YESU tunakuwa na ROHO MTAKATIFU  ambaye hutufanya kuchukia dhambi kwani  bila ROHO MTAKATIFU hakuna awezaye kuacha dhambi.
BIBLIA katika Yohana 3:3 ‘’YESU akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa MUNGU. ‘’
 
*Kuzaliwa mara ya pili ni 

1: Kumwamini YESU.

2: Kubatizwa .

3: Kuwa na ROHO MTAKATIFU.

Yohana 3:17-18’’ 
Maana MUNGU hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Amwaminiye yeye hahukumiwi; asiyeamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa MUNGU. ‘’
 
Tunaokoka hapa hapa duniani kwa sababu ‘’ 
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya KRISTO amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. ‘’- 2 Korintho 5:17.
 
*Ndugu ukiamua kuokoka usirudi nyuma maana unaweza ukapoteza wokovu wako.Luka 9:61-62''
Mtu mwingine pia akamwambia, BWANA, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. YESU akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa MUNGU.'' 
*Watu wengine huogopa kuacha dhambi  eti kwa sababu shetani atawatesa kwa sababu wamewahi kuingia maagano naye ya kishetani huo ni uongo. Maana YESU akikuokoa anakuhamisha kutoka katika kila agano lako na shetani na kuanzia muda hu unakua mtoto wa MUNGU ambaye huwezi kurogwa tena maana mamlaka ya BABA yako wa mbinguni uliyeamua kumpa maisha yako ni kuu sana na hakuna anayeweza kukudhuru tena.na BWANA YESU atakuwa ndiye anayekuchunga Zaburi 23:1’’ BWANA ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu. ‘’ .
 
*Ndugu  duiniani hapa tunapita tu maana hata kama ukiishi miaka 98 hapa duniani lakini ni bure kabisa kama utapotelea motoni baada ya kufa kwa hiyo bora kumpa YESU maisha yako na utakuwa huru kabisa pia utapata uzima sasa na baadae uzima tele. YESU anasema katika Yohana 10:10b’’
mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. ‘’.
ndugu dunia hii tuliikuta na tutaiacha hivyo ni heri kwa sasa kuishi maisha ya kumcha MUNGU. Neno la MUNGU linakushauri kwamba ‘’
Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.  Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya MUNGU adumu hata milele. ‘’-1 Yohana 2:15-17

MUNGU akubariki sana
Ni mimi ndugu yako Peter Michael Mabula.

USINGIZI WA KIROHO * sehemu ya tatu*

Na mtumishi Gasper Madumla


Bwana Yesu asifiwe…
Karibu tuendelee…

KULALA KIROHO
*Ni ile hali ya kujisahau kufanya mazoezi ya UTAUWA
( hali ya kujisahau kukaa katika uwepo wa Bwana.)

*Mtu yeyote Yule asiyekaa ndani ya UWEPO wa Mungu basi ni dhahili kabisa atakuwa katika UWEPO wa shetani

Kwa jambo hilo hakuna hali ya uvugu uvugu,yaani ikiwa mtu hatakuwepo katika ufalme wa Mungu basi jibu ni kwamba atakuwepo katika ufalme wa shetani,hakuna ufalme wa VUGU VUGU.

Binadamu aliumbwa kwamba akae katika uwepo wa Mungu muda wote,maana hapo ndipo pana maisha ya kweli kama vile samaki akaavyo katika uwepo wa maji.
Endapo utamtoa samaki katika maji basi ujue atakufa tu,alikadhalika kwa mtu ambaye ametolewa katika uwepo wa Mungu ,ujue naye ni lazima afe,afe kifo cha kiroho.

Mtu alipo lala kiroho,aliruhusu Adui aamke na kuja kupanda uwepo wake kwa sababu zipo falme mbili hapa Duniani
*Ufalme wa Nuru
*Ufalme wa giza

Labda tuendelee kujifunza juu ya ile habari ya wale makahaba wawili,tuone ilikuwaje;(Kumbuka tulikuwa tumeishia mstari wa 21,katika 1 Wafalme sura ya 3)Sasa tunaendelea na mstari wa 22.

Tunasoma 1 Wafalme 3 :22
“ Ndipo yule mwanamke wa pili akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wangu ndiye aliye hai, na mtoto wako ndiye aliyekufa. Na mwenzake akasema, Sivyo hivyo; bali mtoto wako ndiye aliyekufa, na mtoto wangu ndiye aliye hai. Ndivyo walivyosema mbele ya mfalme.”

*Adui hujaribu kwa KUTUMIA NGUVU ZAKE kubadilisha ukweli kwa uovu juu ya kile ulichopewa na Bwana Mungu.
Tazama andiko hilo vizuri jinsi yule mama ambaye mtoto wake aliyekufa akijaribu kumshindikiza mwenzake akubaliane naye kiwepesi wepesi.

Jiulize ni mara ngapi unabadilishiwa vitu vyako halisi kwa vitu feki,pindi ulalapo kiroho?
Labda unaweza usijue haya mambo kiurahisi maana shetani naye ni mjinga kwa sababu yeye huja kama malaika wa Nuru ili pindi ajapo kukubadilishia mambo yako usimgundue na uone ni sawa tu.

*Lakini leo Sio wakati wa kukubali kiurahisi rahisi tu.

Oooh,!
Jina la Bwana libarikiwe sana…

Nampenda yule mama mwenye haki,Kwa maana alisema HAPANA! si kweli katika maelezo ya ADUI alipeleka naye maelezo yake mbele ya mfalme.
Leo tunaye mfalme wetu,Pindi uonapo mambo si shwari baada ya mbadilishano uliotokea usiku,
nawe usisite kwenda mbele ya mfalme ambaye ndie YESU KRISTO WA NAZARETI

Nakuambia mpelekee mashtaka yako,peleka na kile kilichobadilishwa tena mpeleke na huyo adui/shetani mwambie twende msalabani tukashtaki,
kisha uone.

Katika mstari wa 23
Tunasoma ;
1 Wafalme 3 :25
“ Mfalme akasema, Mkate mtoto aliye hai vipande viwili, kampe huyu nusu, na huyu nusu.”

*Hapa tunajifunza kwamba,Mfalme wetu Bwana Yesu ,mfalme wa Amani yeye hana upendeleo ,Yeye huamua kwa HAKI kwa maana yeye ni mwenye haki na mtakatifu sana.

Adui alifurahia sana kusikia mtoto yule aliye hai kwamba atakatwa kwa upanga hadi kufa.
Kwa maana alijua kwamba watakosa wote.Lengo lake ni kunyang’anya mtoto ambaye si wake.

*
Na hivi ndivyo hali ilivyo kwa shetani katika maisha yetu kila siku .Yeye shetani/Adui hufurahia pale unapopoteza kile kizuri.
Lakini ninakuambia Mungu wetu ambaye ni mfalme Yeye atahukumu kwa haki tu,
Tazama ikiwa Adui ameshika tumbo lako katika ulimwengu wa roho kwa kukubadilishia KIZAZI kwamba USIZAE,Leo hii ninakutangazia UTAZAA katika jina la Yesu Kristo,ni jambo la kuamini tu,na inawezekana.

Kumbuka ;
Watu hao ni makahaba tu ,
watu waliohasi mbele za Bwana
Lakini Biblia inasema walimuendea mfalme kwa ajili ya kupata haki.

*Hata wewe uliye mdhambi leo ninakuambia bado ipo nafasi ya kumuendea Bwana Mfalme kwa kuomba TOBA kisha kumpelekea mashtaka yako uliyobadilishiwa wakati ulipokuwa katika ufalme wa giza,kwa maana ulipokuwa umelala kiroho ndio kipindi ulipokuwa katika ufalme wa giza.

*Ikiwa makahaba walimuendea Bwana naye Bwana akaamua kwa haki, JE SI ZAIDI SANA KWAKO WEWE AMBAYE SI KAHABA?

*ninakuomba usikose kabisa fundisho hili katika sehemu ya nne,
maana natamani hata kama ning’eliweza kuongea na wewe moja kwa moja,Nitakapomaliza fundisho hili nitafanya maombi kwako ukiwa utahitaji mawasiliano 0655 111149

ITAENDELEA…

UBARIKIWE.

UMUHIMU WA KIJANA KUWEPO KANISANI






JEREMIA 1: 4 – 10


Ø Ulishawahi kujiuliza ulizaliwa kwa kusudi gani?

Ø Ujana ni zawadi kutoka kwa Mungu.


Ø Mungu anajua umuhimu wa Kijana na shetani anajua umuhimu wake pia.


Ø Ili kuleta mafanikio na matokeo ya haraka Kijana ana uwezo mkubwa sana.


Ø Ni silaha nyepesi mno na hatari sana.


Ø Mungu anamtuma Yesu katika umri wa ujana na matokeo yake ni makubwa sana.



UMUHIMU WA KIJANA KATIKA JAMII:


a.      Kutatua tatizo ndani ya jamii (1Samw, 17: 31-33, 46-51)

b.     Kurudisha matumaini (Esta, 4: 12-16, 7: 1-10

c.      Kurekebisha hali ya mambo (Mwanzo 41: 34 – 44)

d.     Kurudisha heshima iliyopotea katika jamii.



UMUHIMU WA KIJANA KANISANI (Math, 1: 18 – 21)


a.      Kujishughulisha na mambo ya Kanisani kwake, kuwaza jinsi kutakavyopendeza.


b.     Kujishughulisha na Baba yake wa Kiroho (Mchungaji) 2Tim, 1: 2 – 4.


c.      Kuomba juu ya Kanisa / kufundisha / kuwaleta watu kwa Yesu.


d.     Kuwa mkarimu Kanisani na nyumbani, Mf, Rebeka,Mariamu, Mwanzo 24: 13 -26.


e.      Kujitolea kifedha,Kiakili ,Muda (Mf, Dorkasi, Warumi 12: 1)

v Kanisa lenye nguvu ni lile Vijana wao wanajitambua.


v Kanisa lenye matokeo mazuri linatokana na Familia zinazolijenga Kanisa.

v Kijana akikosa mwelekeo anaharibu mwelekeo mzima wa Kanisa.

v Vijana wachache tu wanaweza kuleta mabadiliko makubwa sana Mf, Vijana watatu (3) Shedraki, Meshaki na Abednego (Danieli 3: 16 – 19 mst 28 -30.


v Kijana aliyebadilika moyoni mmoja tu anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana, Mf, Danieli 6: 24 – 28.


v Alionyesha Mungu wake na Mfalme na jamii yote ikamwinamia Mungu wake.


v Biblia inasema mtu asiudharau ujana wako, 1Tim, 4: 12.


v Kijana asipojitambua na kuwajibika atadharauliwa tu kama hakuna kitu umekifanya Kanisani kwako kinachoonekana.


v Una ulichokifanya kwa Baba yako wa Kiroho? (Mchungaji).


v Una ulichokifanya katika jamii ya kwenu?.


v Penda kijana ukiwepo mahali uwepo kwa faida, usiwe hasara bali uwe faida.


v Huwezi kuheshimiwa kama hakuna kitu unachomfaidisha nacho Mungu.


v Kijana Joshua alikabidhiwa jukumu la kuwaingiza watu Kanaani kwani alikuwa Kijana aliyejituma, aliye tayari anayepatikana, (Hesabu, 27: 18, Kutoka, 17: 8 – 10).

MUNGU awabariki sana

By Bishop YONA   P  SOLA LEMA
Kanisa la SAFINA VICTORY PENTECOSTAL
Ungalimited, Arusha
0754049163.
karibu kwa maombezi na ushauri wa kibiblia.